Utangulizi Wa Elimu Ya Kuitetea Imani
Maelezo ya kozi
Kozi hii inafundisha misingi ya kisayansi, kihistoria, na kifalsafa kwa mtazamo wa ulimwengu wa Kikristo, na inaonyesha jinsi gani imani ya Kikristo ni thabiti katika hoja na hali halisi.
Malengo ya kozi
(1) Kuelewa uhusiano uliopo kati ya Elimu ya Kuitetea imani na Injili. (Somo la 1)
(2) Kujibu hoja potofu zinazohusiana na Elimu ya Kuitetea imani. (Somo la 2)
(3) Kuelewa ushahidi uliopo kuhusiana na uwepo wa Mungu (Somo la 3)
(4) Kuthamini ushahidi wa uumbaji (Somo la 4)
(5) Kukariri hoja za ujumla kuhusiana na ukweli wa Ukristo (Somo la 5)
(6) Kutambua ushahidi wa kuaminika kwa Agano Jipya (Somo la 6)
(7) Kuthamini umuhimu wa kutimia kwa unabii kuhusiana na Uungu wa Yesu (Somo la 7)
(8) Kutathmini ushahidi wa ufufuo wa Yesu Kristo (Somo la 7)
(9) Kuyaelewa madai ya Yesu ya Uungu, na mwitikio unaofaa kwa madai hayo (Somo la 8)
(10) Kujibu maswali yanayohusu upekee wa imani ya Kikristo, imani ya Utatu Mtakatifu, imani kuwa vitu vyote (miti, mawe upepo n.k.) vina roho, na hatima ya wale ambao hawajawahi kuisikia Injili (Somo la 9)
Mada za somo
Utangulizi wa Elimu ya Kuitetea Imani
Dhana potofu dhidi ya Elimu ya Kuitetea Imani
Je, Mungu Yupo?
Elimu ya Kuitetea Imani ya Uumbaji
Hoja za Ujumla kuhusu Imani ya Kikristo
Kuaminika kwa Agano Jipya
Unabii wa Masihi na Ufufuo
Madai ya Yesu kuwa Yeye ni Mungu
Upekee wa Ukristo katika Dini Nyingi